Na 11
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,
2022
taarifa chini ya kifungu kidogo cha (4), Tume itazingatia
idadi ya watu ambao watapaswa kuarifiwa.
Kurekebisha,
kuzuia, kufuta
na kuharibu
taarifa binafsi
38.-(1) Pale ambapo Tume itaridhika kwa maombi
ya mhusika wa taarifa kuwa taarifa binafsi zinazomhusu
mhusika huyo siyo sahihi, Tume inaweza kumuamuru
mkusanyaji au mchakataji kurekebisha, kuzuia, kufuta au
kuharibu taarifa hizo.
(2) Kifungu kidogo cha (1) kitatumika hata kama
taarifa binafsi ni kumbukumbu sahihi zilizopokelewa na
mkusanyaji au mchakataji kutoka kwa mhusika wa taarifa
au mtu mwingine.
(3) Pale ambapo taarifa binafsi siyo sahihi, Tume
inaweza kumuelekeza mkusanyaji au mchakataji
kurekebisha taarifa hizo kwa kadri itakavyoona inafaa.
(4) Pale ambapo taarifa binafsi zinazolalamikiwa
zimerekebishwa, zimezuiwa, zimehuishwa, zimefutwa au
zimeharibiwa chini ya kifungu hiki, mkusanyaji au
mchakataji atatakiwa kuwataarifu wahusika wengine
ambao walipatiwa taarifa binafsi husika kuhusu
kurekebishwa, kuzuiwa, kuhuishwa, kufutwa au
kuharibiwa kwa taarifa hizo.
SEHEMU YA SABA
UCHUNGUZI WA MALALAMIKO
Malalamiko
dhidi ya
ukiukwaji wa
misingi ya
ulinzi wa taarifa
binafsi
Notisi ya
39.-(1) Mtu yeyote atakayebaini kuwa mkusanyaji au
mchakataji amekiuka misingi ya ulinzi wa taarifa binafsi
anaweza kuwasilisha malalamiko kwa Tume.
(2) Pale ambapo Tume imejiridhisha kuwa kuna
sababu za msingi za kuchunguza suala chini ya Sheria hii,
Tume inaweza kuanzisha uchunguzi wa malalamiko
kuhusiana na suala hilo.
(3) Malalamiko yatakayowasilishwa katika kifungu
hiki yatachunguzwa na kumalizika ndani ya siku tisini
tangu tarehe ya kupokelewa.
(4) Tume inaweza, kwa kuzingatia mazingira ya
malalamiko, kuongeza muda ulioainishwa chini ya kifungu
kidogo cha (3) kwa kipindi kisichozidi siku tisini.
40. Kabla ya kuanza uchunguzi wa malalamiko chini
23
اختر الفقرة المستهدفة3
الاتصال بفقرة
Connect to an entity
Disable highlights
أضف إلى جدول المحتويات