Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 (e) kuwapa wahusika wa taarifa haki na nafuu katika kulinda taarifa binafsi kutokana na ukusanyaji na uchakataji usiofuata masharti ya Sheria hii. Misingi ya ulinzi wa taarifa binafsi 5. Mkusanyaji au mchakataji atahakikisha kwamba taarifa binafsi(a) zinachakatwa kihalali, kwa haki na kwa uwazi; (b) zinakusanywa kwa madhumuni mahususi, yaliyobainishwa na halali, na taarifa hizo hazitaendelea kuchakatwa kwa namna tofauti na madhumuni yaliyoainishwa; (c) zinatosheleza na ni muhimu kwa madhumuni ya uchakataji kama ilivyokusudiwa; (d) ni sahihi na pale inapobidi, zinaboreshwa kwa kuchukua hatua zote muhimu kuhakikisha taarifa binafsi zisizo sahihi zinafutwa au kurekebishwa bila kuchelewa; (e) zinahifadhiwa katika namna inayoruhusu utambuzi wa mhusika wa taarifa kwa muda usiozidi ule unaohitajika kwa madhumuni ya uchakataji wa taarifa binafsi husika; (f) zinachakatwa kwa kuzingatia haki za mhusika wa taarifa; (g) zinachakatwa kwa namna ambayo itahakikisha usalama wa taarifa binafsi, ikijumuisha ulinzi dhidi ya uchakataji usioruhusiwa au ulio kinyume cha sheria na dhidi ya hasara, uharibifu au madhara yoyote, kwa kutumia hatua sahihi za kiufundi au za kiutawala; na (h) hazisafirishwi nje ya mipaka ya nchi kinyume cha masharti ya Sheria hii. SEHEMU YA PILI TUME YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI Uanzishwaji wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi 6.-(1) Inaanzishwa Tume itakayojulikana kama Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi. (2) Tume itakuwa taasisi nafsi yenye mamlaka ya urithishaji wa kudumu na lakiri yake, na kwa jina lake 8

اختر الفقرة المستهدفة3

الاتصال بفقرة
Connect to an entity
Disable highlights
أضف إلى جدول المحتويات