Na.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 52 (2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua kiasi cha shilingi milioni tatu au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja. Matusi ya kibaguzi 18. -(1) Mtu hatamtukana au kumfedhehesha mtu mwingine kwa kupitia mfumo wa kompyuta, kutokana na sababu kuwa mtu huyo mwingine ni mmoja kati ya kundi linalotambulika kwa tabaka, rangi, asili, utaifa, kabila au dini fulani. (2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja. Mauaji ya kimbari na makosa dhidi ya ubinadamu 19.-(1) Mtu hatachapisha au kusababisha kuchapishwa kinyume na sheria vitu vinavyochochea, kanusha, punguza au halalisha matendo yanasababisha mauaji ya kimbari na makosa dhidi ya ubinadamu kwa kupitia mfumo wa kompyuta. (2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni kumi au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja. (3) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, tafsiri ya “mauaji ya kimbari” itakuwa na maana kama ilivyo tafsiriwa katika Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari wa mwaka 1948.

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents