Na.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 62 Amri ya mahakama 36. Endapo ambapo utoaji data au utunzaji data wa dharura chini ya vifungu vya 31, 32, 33, 34 au 35 kwa kadri itakavyokuwa, hauwezi kufanyika bila kutumia nguvu au kutokana na pingamizi kutoka kwa mtu mwenye kumiliki data au thamani ya ushahidi katika data inaweza kuhifadhiwa kwa amri ya mahakama, afisa utekelezaji wa sheria anaweza kuomba mahakamani amri ya utoaji au utunzaji wa data. Matumizi ya kifaa cha TEHAMA katika uchunguzi 37.-(1) Endapo afisa utekelezaji wa sheria anaridhika kuwa ushahidi wa msingi hauwezi kukusanywa kwa kutumia utaratibu ulioainishwa chini ya Sehemu hii, afisa utekelezaji huyo anaweza kuiomba mahakama kutoa amri ya kuidhinisha matumizi ya kifaa cha uchunguzi. (2 ) Maombi yaliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha ( 1) yatajumuisha(a) jina na anwani ya mtuhumiwa; (b) maelezo ya mfumo wa kompyuta unaolengwa; na (c) maelezo ya hatua zinazokusudiwa kuchukuliwa, madhumuni, kiasi na muda wa matumizi unaokusudiwa. (3) Afisa utekelezaji wa sheria atahakikisha kuwa mabadiliko yaliyofanywa kwenye mfumo wa kompyuta au data iliyomo kwenye kompyuta ya mtuhumiwa zinajikita kwenye marekebisho yaliyo ya msingi kwa ajili ya uchunguzi na kwamba mabadiliko yoyote yanayorudishwabaada ya kukamilika kwa uchunguzi. (4) Wakati wa uchunguzi, afisa utekelezaji wa sheria ataingiza: (a) mbinu za kiufundi zilizotumika, muda na terehe ya maombi; (b) utambuzi wa mfumo wa kompyuta na maelezo ya mabadiliko yaliyofanyika wakati wa uchunguzi;

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents