63 No.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 uchunguzi; (c) taarifa yoyote iliyopatikana; (5) Taarifa iliyopatikana chini ya kifungu hiki italindwa dhidi ya mabadiliko, kufutwa bila ya idhini na kuingia kwenye mfumo bila idhini. (6) Idhini iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (1) itakuwa halali kwa kipindi cha siku kumi na nne. (7) Mahakama inaweza, kwa maombi, kuongeza muda uliotolewa chini ya kifungu kidogo cha (6) kwa kipindi kingine cha siku kumi na nne au kwa kipindi kingine kwa kadri itakavyoona inafaa. (8) Iwapo mchakato wa uwekaji wa kifaa unahitaji kutembelea eneo, masharti ya kifungu cha 30 yatatumika. (9) Pamoja na amri iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (1), mahakama inaweza, kwa maombi, kumuamuru mtoa huduma kuwezesha mchakato wa kuweka kifaa cha kipelelezi. (10) Waziri anaweza, kwa taarifa itakayochapishwa kwenye Gazeti la Serikali, kuainisha makosa ambayo mahakama inaweza kutoa amri ya kutumia kifaa cha TEHAMA katika uchunguzi. Usikilizaji wa maombi 38. Utaratibu wa kusikiliza maombi kwa mujibu wa Sehemu hii utafanywa kwa upande mmoja na kwa siri. SEHEMU YA TANO WAJIBU WA WATOA HUDUMA Wajibu wa ufuatiliaji 39.-(1) Wakati wa kutoa huduma chini ya Sehemu hii, mtoa huduma(a) hatawajibika kufuatilia data ambayo

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents