Na 11
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,
2022
taarifa atawasilisha maombi ya usajili kwa Tume.
(3) Tume inaweza, katika muda utakaoainishwa
katika
kanuni,
kukubali
au
kukataa
maombi
yaliyowasilishwa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (2).
(4) Tume itatoa cheti cha usajili kwa mkusanyaji au
mchakataji aliyekidhi matakwa ya usajili na kusajiliwa
chini ya kifungu hiki.
(5) Endapo Tume itakataa maombi ya usajili
itapaswa kumtaarifu mwombaji kwa maandishi juu ya
uamuzi wake na sababu ya uamuzi huo.
Rejesta ya
wakusanyaji na
wachakataji
15.-(1) Tume itaanzisha na kutunza rejesta ya
wakusanyaji na wachakataji waliosajiliwa kwa mujibu wa
Sheria hii.
(2) Rejesta ya wakusanyaji na wachakataji
itajumuisha taarifa kama itakavyoainishwa katika kanuni.
(3) Mkusanyaji au mchakataji anaweza, wakati
wowote, kuomba kwa Tume kuhuisha au kubadili taarifa
yoyote iliyoingizwa katika rejesta.
Kipindi cha
usajili
16.-(1) Kipindi cha usajili kitakuwa ni miaka mitano
kuanzia tarehe ya kutolewa kwa cheti cha usajili.
(2) Maombi ya kuhuisha usajili yatawasilishwa
ndani ya kipindi cha miezi mitatu kabla ya tarehe ya kuisha
kwa kipindi cha usajili kama itakavyoainishwa katika
kanuni.
Ukaguzi wa
taarifa
zilizosajiliwa
17. Kwa kuzingatia utaratibu utakaoainishwa kwenye
kanuni na baada ya kulipwa kwa ada iliyoainishwa, Tume
inaweza kuruhusu mtu yeyote kupekua na kupakua taarifa
yoyote iliyoingizwa katika rejesta.
Kufutwa kwa
usajili
18. Tume inaweza kufuta usajili uliofanyika chini ya
Sheria hii kwa utaratibu utakaoainishwa katika kanuni.
Makosa
yanayohusiana
na usajili
19. Mtu atakayekiuka masharti ya Sehemu hii au kutoa
taarifa za uongo au za kupotosha wakati wa usajili au
uhuishaji anatenda kosa na endapo atatiwa hatiani
atawajibika kwa adhabu iliyoainishwa katika kifungu cha
63.
20. Mtu yeyote ambaye hataridhika na uamuzi wa
Rufaa
kuhusiana na
12
Select target paragraph3
Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents