Na 11 Sura ya 13 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 majukumu yaliyoainishwa katika Sheria hii; “kanuni za maadili” maana yake ni kanuni zinazobainisha maadili na miiko ya wachakataji na wakusanyaji wa taarifa binafsi zinazoandaliwa kwa mujibu wa kifungu cha 65; “mahakama” maana yake ni mahakama yenye mamlaka ya kusikiliza suala husika; “mchakataji” maana yake ni mtu, taasisi nafsi au taasisi ya umma ambayo inachakata taarifa binafsi kwa ajili na kwa niaba ya mkusanyaji chini ya maelekezo ya mkusanyaji, isipokuwa kwa watu ambao, chini ya mamlaka ya moja kwa moja ya mkusanyaji, wanaruhusiwa kuchakata taarifa binafsi, na itajumuisha mwakilishi wake; “mhusika wa taarifa” maana yake ni mhusika wa taarifa binafsi zinazochakatwa kwa mujibu wa Sheria hii; “Mkurugenzi Mkuu” maana yake ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume aliyeteuliwa chini ya kifungu cha 11; “mkusanyaji” maana yake ni mtu, taasisi nafsi au taasisi ya umma ambayo peke yake au kwa pamoja na taasisi nyingine huamua madhumuni na njia za uchakataji wa taarifa binafsi; na pale ambapo madhumuni na njia za uchakataji zimebainishwa katika sheria, “mkusanyaji” ni mtu, taasisi nafsi au taasisi ya umma iliyoteuliwa kwa mujibu wa sheria na itajumuisha mwakilishi wake; “mpokeaji” maana yake ni mtu, taasisi nafsi, taasisi ya umma au mtu mwingine yeyote ambaye anapokea taarifa binafsi kutoka kwa mkusanyaji; “mtaalamu wa afya” maana yake ni mtu anayetoa huduma za afya na kutambuliwa hivyo kwa mujibu wa sheria; “mtoto” ina maana kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Mtoto; “mtu mwingine” maana yake ni mtu, taasisi nafsi au taasisi ya umma tofauti na(a) mhusika wa taarifa; (b) mkusanyaji au mchakataji; na (c) mtu yeyote aliyepewa mamlaka ya kuchakata 5

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents