Na.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 40 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA.14 YA 2015 NAKUBALI, JAKAYA MRISHO KIKWETE Rais 25 Aprili, 2015 Sheria inayoainisha masharti yanayohusu makosa yanayohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano; kuainisha utaratibu wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa kielektroniki na masuala mengine yanayohusiana na hayo. [................] IMETUNGWA na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI Jina na tarehe ya kuanza kutumika 1. Sheria hii itaitwa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, na itaanza kutumika tarehe ambayo Waziri, kwa Tanzago la Serikali katika Gazeti la Serikali. Matumizi 2. Isipokuwa kwa kifungu cha 50, Sheria hii itatumika Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents