59 No.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 (iii) kuongeza wigo wa upekuzi au uwezo wa kuingia kwenye mfumo mwingine iwapo afisa utekelezaji wa sheria anayefanya upekuzi ana sababu za kuaminika kuwa data inayotafutwa, inatunzwa kwenye mfumo mwingine wa kompyuta au sehemu yake. (2) Upekuzi chini ya kifungu hiki utafanyika kwa mujibu wa sheria zinazosimamia masuala ya upekuzi na ukamataji wa mali. (3) Endapo kifaa au mfumo wa kompyuta umeondolewa au hauingiliki kutokana na upekuzi au ukamataji wa mali, afisa utekelezaji wa sheria, wakati wa upekuzi na ukamataji wa mali au mara tu baada ya upekuzi(a) ataandaa orodha ya vitu vilivyokamatwa au kufanywa visiingilike, muda ambao mali ilikamatwa; (b) atampatia nakala ya orodha ya mali iliyokamatwa mtu anayemiliki au mwangalizi wa mfumo husika wa kompyuta. (4) Mtu anayemiliki au mwangalizi wa mfumo wa kompyuta anaweza kumuomba afisa utekelezaji wa sheria ruhusa ya kuingia au kudurufu taarifa zilizopo kwenye mfumo wa kompyuta baada ya ukamataji wa mali. (5) Bila ya kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (4), afisa utekelezaji wa sheria anaweza kukataa kuruhusu kuingia kwenye mfumo au kudurufu taarifa iwapo ana sababu za msingi za kuamini kuwa kuruhusu kuingia au kudurufu taarifa(a) itakuwa ni kosa; au (b) kutaathiri(i) uchunguzi unaohusiana na upekuzi; (ii) upelelezi mwingine unaoendelea; au

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents