Na.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 56 (a) isipokuwa kwa kiasi cha adhabu, iwapo(i) mkosaji anatenda yote ambayo ni muhimu kwa utendaji wa kosa; au (ii) utekelezaji wa kusudio lake kwa ukamilifu unazuiliwa na mazingira ambayo hayaingiliani na kusudio lake; au (iii) anaacha kutekeleza kusudio lake kwa hiari yake mwenyewe; (b) kutokana na sababu za mazingira yasiyojulikana kwa mhalifu, haiwezekani kutenda kosa. (3) Mtu yeyote anayejaribu kutenda kosa chini ya Sheria hii atakua ametenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni moja au kifungo kwa kipindi kisichopungua miezi sita au vyote kwa pamoja. Kula njama ya kutenda kosa 27. Mtu yeyote anayekula njama na mtu mwingine kutenda kosa chini ya Sheria hii, anatenda kosa na iwapo atatiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni moja au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja. Ulinzi wa miundombinu muhimu ya TEHAMA 28. -(1) Waziri anaweza, kwa amri itakayochapishwa kwenye Gazeti la Serikali kuainisha mifumo ya kompyuta kama miundombinu muhimu. (2) Amri iliyorejewa chini ya kifungu kidogo cha (1) inaweza kuainisha miongozo au taratibu zinazohusu (a) usajili, ulinzi au utunzaji wa miundombinu muhimu; (b) usimamizi wa jumla wa miundombinu muhimu; (c) kuingia, kuhamisha na kudhibiti data kwenye miundombinu muhimu; (d) uwepo wa audilifu au uhalali wa data au taarifa zilizo katika miundombinu muhimu;

Seleccionar párrafo de destino3

Conectar a un párrafo
Connect to an entity
Disable highlights
Añadir a la tabla de contenidos