57 No.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 (e) njia zitakazotumika kuhifadhi au kutunza data au taarifa kwenye miundombinu muhimu; (f) mipango ya kudhibiti majanga iwapo kutatokea uharibifu kwenye miundombinu muhimu au sehemu yake; (g) namna na utaratibu wa kuendesha ukaguzi kwenye miundombinu muhimu yoyote; (h) jambo jingine lolote ambalo ni muhimu kwa ulinzi, usimamizi na udhibiti wa data na rasimali nyingine kwenye miundombinu muhimu. (3) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, “miundombinu muhimu ya TEHAMA” inajumuisha mali, vifaa, mifumo ya kompyuta au mitandao inayoshikika na isiyoshikika ambayo ina umuhimu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kiasi kwamba kutokufanya kazi kwake kuna madhara ya kiusalama, kiuchumi na kijamii. Makosa yanayohusu miundombinu muhimu ya TEHAMA 29. Endapo mtu anatenda kosa chini ya Sheria hii au sheria nyingine yoyote linalohusiana na miundombinu muhimu, mtu huyo atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shillingi milioni mia moja au mara tatu ya hasara aliyoisababisha au kifungo kisichopungua miaka mitano au vyote kwa pamoja. SEHEMU YA TATU MAMLAKA YA MAHAKAMA Mamlaka ya mahakama 30. -(1) Mahakama zitakuwa na uwezo wa kusikiliza shauri lolote chini ya Sheria hii pale ambapo kosa au sehemu ya kosa (a) limetendeka ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; (b) limetendeka kwenye meli au ndege iliyosajiliwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

Seleccionar párrafo de destino3

Conectar a un párrafo
Connect to an entity
Disable highlights
Añadir a la tabla de contenidos