Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 inayomhusu ikiwa uchakataji huo unaweza kusababisha madhara makubwa kwake au kwa mtu mwingine. (2) Kifungu kidogo cha (1) hakitatumika katika mazingira yaliyoondolewa katika mawanda ya masharti ya Sheria hii. Haki ya kuzuia uchakataji wa taarifa binafsi kutumika kwa madhumuni ya utangazaji wa biashara 35.-(1) Mhusika wa taarifa, kwa kuzingatia utaratibu utakaoainishwa kwenye kanuni, anaweza kumtaka mkusanyaji kuacha kuchakata taarifa zake binafsi kwa madhumuni ya matangazo ya biashara. (2) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (1), mhusika wa taarifa anaweza kuingia mkataba na mkusanyaji kwa madhumuni ya kutumia au kuchakata taarifa zake binafsi kwa ajili ya kunufaika kifedha. (3) Katika kifungu hiki “matangazo ya biashara” yanajumuisha wasilisho, kwa namna yoyote, ya tangazo la kibiashara linaloelekezwa kwa mtu fulani. Haki kuhusiana na uamuzi unaofanywa kiotomatiki 36.-(1) Mhusika wa taarifa anaweza, kupitia utaratibu utakaoainishwa kwenye kanuni, kumtaka mkusanyaji kuhakikisha kwamba uamuzi wowote unaofanywa na mkusanyaji au kwa niaba ya mkusanyaji ambao una athari kubwa kwa mhusika wa taarifa, hautegemei uchakataji kwa njia ya kiotomatiki pekee. (2) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1), pale ambapo uamuzi wenye athari kubwa kwa mhusika wa taarifa unategemea uchakataji wa kiotomatiki pekee(a) mkusanyaji atalazimika mapema iwezekanavyo kumtaarifu mhusika wa taarifa kwamba uamuzi ulichukuliwa kwa kutegemea uchakataji wa kiotomatiki; na (b) mhusika wa taarifa anaweza kumtaka mkusanyaji kushughulikia upya uamuzi. (3) Kifungu hiki hakitatumika ikiwa uamuzi uliofanywa(a) ni muhimu kwa ajili ya kuingia au kutekeleza mikataba kati ya mhusika wa taarifa na mkusanyaji; (b) umeruhusiwa na sheria yoyote; 21

Seleccionar párrafo de destino3

Conectar a un párrafo
Connect to an entity
Disable highlights
Añadir a la tabla de contenidos