Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 (c) ni kutokana na ridhaa iliyotolewa na mhusika wa taarifa. Haki ya fidia 37.-(1) Mhusika wa taarifa atakayepata madhara kwa sababu za ukiukwaji wa masharti ya Sheria hii uliofanywa na mkusanyaji au mchakataji atakuwa na haki ya kulipwa fidia kutoka kwa mkusanyaji au mchakataji kutokana na madhara hayo. (2) Mhusika wa taarifa ambaye haki zake zimevunjwa kwa sababu ya ukiukwaji wa masharti yoyote ya Sheria hii atakuwa na haki ya kulipwa fidia kutoka kwa mkusanyaji au mchakataji ikiwa(a) mlalamikaji ndiye mhusika wa taarifa aliyeathiriwa au mwakilishi wa mhusika wa taarifa ikiwa mhusika ni mtoto au mtu asiye na akili timamu; (b) haki za mhusika wa taarifa zimevunjwa kwa sababu ya ukiukwaji huo; na (c) athari hizo zinahusiana na uchakataji wa taarifa binafsi kinyume na masharti ya Sheria hii. (3) Endapo Tume itajiridhisha na maombi ya mhusika wa taarifa(a) kwamba amepata madhara kwa sababu ya ukiukwaji wa masharti ya Sheria hii uliofanywa na mkusanyaji au mchakataji kuhusiana na taarifa binafsi yoyote, katika mazingira yanayompatia haki ya kulipwa fidia chini ya kifungu hiki; na (b) kwamba kuna hatari kubwa ya ukiukwaji zaidi kuhusiana na taarifa binafsi husika katika mazingira hayo, Tume inaweza kuamuru kurekebishwa, kuzuiwa, kufutwa au kuharibiwa kwa taarifa hizo. (4) Tume, pale ambapo imetoa amri chini ya kifungu kidogo cha (3) na endapo itaona kuwa ni busara, inaweza kumuamuru mkusanyaji au mchakataji kuwajulisha wahusika wengine ambao wamepatiwa taarifa binafsi kuhusu marekebisho, zuio, ufutaji au uharibifu wa taarifa hizo. (5) Katika kuamua endapo ni sahihi kuhitaji 22

Seleccionar párrafo de destino3

Conectar a un párrafo
Connect to an entity
Disable highlights
Añadir a la tabla de contenidos