Na.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 44 “afisa utekelezaji wa sheria” maana yake ni afisa wa polisi mwenye cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa polisi,au cheo cha juu ya hicho au mpelelezi, afisa Usalama wa Taifa mwendesha mashtaka, au afisa muidhiniwa wa mamlaka yenye dhamana na mawasiliano au mtu mwingine yeyote aliyeidhinishwa chini ya sheria yoyote; “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana na masuala ya Habari na Teknolojia ya Habari. “kuchapisha” maana yake ni usambazaji, uwasilishaji, uwekaji wazi, ubadilishanaji,uchapishaji, uonyeshaji, nakili, uuzaji au utoaji kwa ajili ya mauzo, kukodisha au usambazaji wa aina yoyote ile; “mali” maana yake ni mali ya aina yoyote inayotembelea au la, inayogusika au isiyogusika na inajumusha: (a) fedha yoyote inayotumika au isiyotumika katika Jamhuri ya Muungano Tanzania; (b) taarifa, ikijumuisha programu unayotolewa kielektroniki, data au nakala zake, zinazoweza kusomwa na binadamu au kwa kompyuta; au (c) haki yoyote au maslahi kwenye mali; “ubaguzi” maana yake ni taarifa za namna yoyote zinazokuza au kuchochea chuki, ubaguzi au vurugu dhidi ya mtu yeyote au kundi la watu kwa msingi wa tabaka, rangi, asili,utaifa, kabila au dini; “mtoa huduma” maana yeke ni mtu au upande unaowezesha mfumo wa taarifa kupatikana kwa mtu wa tatu.

Sélectionner le paragraphe cible3

Se connecter à un paragraphe
Connect to an entity
Disable highlights
Ajouter à la table des matières