45 No.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 SEHEMU YA PILI MASHARTI YANAYOHUSIANA NA MAKOSA NA ADHABU Kuingia kinyume cha sheria 4.-(1) Mtu hataingia au kusababisha kuingiliwa mfumo wa kompyuta kinyume cha sheria na kwa makusudi. (2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria au yoyote iliyokubwa, au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja. Matumizi ya mfumo wa kompyuta kinyume cha sheria 5.-(1) Mtu hatatumia au kuendelea kutumia mfumo wa kompyuta, kinyume cha sheria na kwa makusudi, baada ya kuisha kwa muda ambao aliruhusiwa kutumia mfumo wa kompyuta. (2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni moja au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria au yoyote iliyokubwa, au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miezi sita au vyote. Kuingilia mawasiliano kinyume cha sheria 6.-(1) Mtu ambaye, kwa makusudi na kinyume cha sheria(a) anaingilia kwa kutumia njia ya kiufundi au kwa njia nyingine yoyote: (i) mawasiliano yasiyo ya umma kwenda au kutoka au yaliyo ndani ya mfumo wa kompyuta;

Sélectionner le paragraphe cible3

Se connecter à un paragraphe
Connect to an entity
Disable highlights
Ajouter à la table des matières