Na 11
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,
2022
sheria zake, ikiwa mkusanyaji ataihakikishia Tume
kwamba kuna ulinzi wa kutosha wa taarifa binafsi, uhuru
na haki za msingi za mhusika wa taarifa, na utekelezaji wa
haki za mhusika wa taarifa, na kwamba ulinzi huo
unaweza kutekelezwa kupitia hatua zinazojitosheleza za
kisheria, kiusalama na masharti husika ya mkataba.
SEHEMU YA SITA
HAKI ZA WAHUSIKA WA TAARIFA
Haki ya kupata
taarifa binafsi
33.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya Sheria hii,
mhusika wa taarifa ana haki ya(a) kufahamishwa na mkusanyaji yeyote endapo
taarifa binafsi zinachakatwa na mkusanyaji
huyo au mkusanyaji mwingine kwa niaba ya
mkusanyaji huyo;
(b) kupewa na mkusanyaji maelezo ya(i) taarifa binafsi zinazomhusu;
(ii) madhumuni ya uchakataji; na
(iii) wapokeaji au makundi ya wapokeaji
waliopewa au wanaoweza kupewa taarifa
hizo;
(c) pale ambapo uchakataji wa taarifa binafsi kwa
njia ya kiotomatiki
kwa madhumuni ya
kutathmini masuala yanayomhusu, umetumika
au unaweza kutumika kama msingi pekee wa
maamuzi yenye athari kubwa kwake,
kufahamishwa na mkusanyaji kuhusu sababu
zilizotumika kufikia uamuzi huo.
(2) Bila kujali masharti ya kifungu kidogo cha (1),
mkusanyaji hatalazimika kutoa taarifa kwa mhusika wa
taarifa endapo taarifa hizo(a) siyo sahihi;
(b) zinahusika katika uchunguzi kwa mujibu wa
sheria; au
(c) zimezuiliwa kwa amri ya mahakama.
Haki ya kuzuia
uchakataji
unaoweza
kumuathiri
mhusika wa
taarifa
34.-(1) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (2),
mhusika wa taarifa ana haki ya kumtaka mkusanyaji
kupitia utaratibu utakaoainishwa katika kanuni, kusitisha
au kutoanza uchakataji wa taarifa binafsi yoyote
20
Sélectionner le paragraphe cible3
Se connecter à un paragraphe
Connect to an entity
Disable highlights
Ajouter à la table des matières