Na 11
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,
2022
inayomhusu ikiwa uchakataji huo unaweza kusababisha
madhara makubwa kwake au kwa mtu mwingine.
(2) Kifungu kidogo cha (1) hakitatumika katika
mazingira yaliyoondolewa katika mawanda ya masharti ya
Sheria hii.
Haki ya kuzuia
uchakataji wa
taarifa binafsi
kutumika kwa
madhumuni ya
utangazaji wa
biashara
35.-(1) Mhusika wa taarifa, kwa kuzingatia utaratibu
utakaoainishwa kwenye kanuni, anaweza kumtaka
mkusanyaji kuacha kuchakata taarifa zake binafsi kwa
madhumuni ya matangazo ya biashara.
(2) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (1),
mhusika wa taarifa anaweza kuingia mkataba na
mkusanyaji kwa madhumuni ya kutumia au kuchakata
taarifa zake binafsi kwa ajili ya kunufaika kifedha.
(3) Katika kifungu hiki “matangazo ya biashara”
yanajumuisha wasilisho, kwa namna yoyote, ya tangazo la
kibiashara linaloelekezwa kwa mtu fulani.
Haki kuhusiana
na uamuzi
unaofanywa
kiotomatiki
36.-(1) Mhusika wa taarifa anaweza, kupitia utaratibu
utakaoainishwa kwenye kanuni, kumtaka mkusanyaji
kuhakikisha kwamba uamuzi wowote unaofanywa na
mkusanyaji au kwa niaba ya mkusanyaji ambao una athari
kubwa kwa mhusika wa taarifa, hautegemei uchakataji
kwa njia ya kiotomatiki pekee.
(2) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha
(1), pale ambapo uamuzi wenye athari kubwa kwa
mhusika wa taarifa unategemea uchakataji wa kiotomatiki
pekee(a) mkusanyaji atalazimika mapema iwezekanavyo
kumtaarifu mhusika wa taarifa kwamba uamuzi
ulichukuliwa kwa kutegemea uchakataji wa
kiotomatiki; na
(b) mhusika wa taarifa anaweza kumtaka
mkusanyaji kushughulikia upya uamuzi.
(3) Kifungu hiki hakitatumika ikiwa uamuzi
uliofanywa(a) ni muhimu kwa ajili ya kuingia au kutekeleza
mikataba kati ya mhusika wa taarifa na
mkusanyaji;
(b) umeruhusiwa na sheria yoyote;
21
Sélectionner le paragraphe cible3
Se connecter à un paragraphe
Connect to an entity
Disable highlights
Ajouter à la table des matières