43 No.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 mfumo wa optika au katika aina nyingine ya mfumo inayofanana na hiyo; “ kifaa cha TEHAMA katika uchunguzi ” maana yake ni kifaa cha uchunguzi au kifaa kinachojumuisha mianzi laini au mianzi ngumu iliyowekwa kwenye au inayohusiana na mfumo wa kompyuta au sehemu ya mfumo wa kompyuta na inayotumika kutekeleza kazi zinazojumuisha uingiaji kwa siri au ukusanyaji wa taarifa za kiuchunguzi zinazohusiana na matumizi ya kompyuta au mfumo wa kompyuta; “zuia” kuhusiana na mfumo wa kompyuta inajumuisha(a) kusababisha kuingiliwa kielektromagnetiki kwa mfumo wa kompyuta; (b) kuvuruga mfumo wa kompyuta, kwa namna yoyote ile; au (c) kuingiza, kutuma, kuzorotesha, kufuta, kuvuruga, kubadilisha au kuzuia data kompyuta; “mtunza data” maana yake ni mtu anayetoa huduma ya kusambaza data kwa kutunza taarifa inayotolewa na mtumiaji wa huduma hiyo; “kiunganishi tovuti” maana yake ni alama, neno, kirai, sentensi au taswira iliyo katika tovuti au taarifa inayokuhusiana na chanzo kingine kinachosababisha kuounyesha au kufunguka kwa tovuti nyingine; “haki bunifu’’ maana yake ni haki zinazotokana au zinazohusiana na haki miliki, hati bunifu, alama za biashara na mambo mengine yanayohusiana nayo; “kuingilia” kuhusiana na utendaji kazi wa kompyuta inajumuisha upatikanaji, utazamaji, usikilizaji au kunukuu data kompyuta yoyote ya mawasiliano ya kompyuta au mifumo ya kompyuta kwa njia yoyote ya kielektroniki;

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents