55 No.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka mitano au vyote, kwa pamoja, pamoja na kulipa fidia kwa mtu aliyeathirika na kosa husika kiasi ambacho mahakama itaona kinafaa Wakosaji wakuu 25. -(1) Mtu yeyote ambaye(a) anafanya kitendo au anaacha kufanya kitendo ambacho kiasi kwamba kutokutenda huko kunasababisha kutendeka kwa kosa; (b) anafanya au anaacha kufanya kitendo kwa madhumuni ya kumwezesha au kumsaidia mtu mwingine kutenda kosa; (c) anamsaidia na kumwezesha mtu mwingine kutenda kosa; (d) anamshawishi au kumlipa mtu mwingine kufanya kosa hilo, atachukuliwa kuwa ameshiriki kutenda kosa na atashitakiwa kama mtu aliyetenda kosa. (2) Mtu anayemlipa mtu mwingine kufanya au kutokufanya kitendo kwa kiasi ambapo, iwapo yeye mwenyewe angefanya kitendo hicho au kutokutenda huko, kitendo hicho kingepelekea kosa kufanyika kwa upande wake na atakuwa na hatia kwa kosa la aina hiyo na atawajibika kwa adhabu sawa kana kwamba yeye mwenyewe angefanya kitendo hicho au kutokutenda huko. Jaribio la kufanya uhalifu 26.-(1) Endapo mtu anakusudia kutenda kosa anaanza kutekeleza kusudio lake na anadhihirisha kusudio lake kwa kitendo kinachoashiria kosa, isipokuwa hatekelezi kusudio lake kwa kiasi cha kutenda kosa hilo, atachukuliwa kuwa ametenda kosa hilo. (2 ) Kwa madhumuni ya kifungu hiki haitakuwa muhimu-

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents