61 No.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 (2) Mahakama inaweza, kwa maombi, kuongezea muda amri chini ya kifungu cha 35 kwa muda ambao itaona unafaa. Utoaji na 34. -(1) Endapo askari polisi mkuu wa kituo au afisa ukusanyaji wa utekelezaji wa sheria mwenye cheo cha askari mkuu wa data nyendo kituo anaridhika kuwa data kompyuta inahitajika kwa madhumuni ya uchunguzi, afisa huyo anaweza kutoa amri kimaandishi kwa ajili ya(a) utoaji au uwekaji kumbukumbu za taarifa za kompyuta zinazohusiana na mawasilano maalum kwa kipindi maalum; au (b) kumruhusu na kumsaidia afisa utekelezaji wa sheria kukusanya aukuwekea kumbukumbu data hizo. (2) Kwa madhumuni ya kifungu hiki “data nyendo” maana yake ni taarifa: (a) inayohusiana na mawasiliano kwa mfumo wa kompyuta; (b) iliyotolewa na mfumo wa kompyuta ambao ni sehemu ya mlolongo wa mawasiliano; na (c) inayoonyesha chanzo cha mawasiliano,njia iliyotumika, muda,ukubwa, uelekeo na aina ya huduma zinazoambatana nazo. Utoaji na 35. Endapo askari polisi mkuu wa kituo au afisa ukusanyaji wa maudhui katika utekelezaji wa sheria mwenye cheo cha askari mkuu wa kituo ana sababu za msingi za kushuku au kuamini kuwa data yaliyomo kwenye mawasiliano ya kielektroniki yanahitajika kwa madhumuni ya uchunguzi, anaweza kutoa amri ya: (a) kukusanya, kurekodi, kuruhusu au kuisaidia mamlaka husika kukusanya au kurekodi taarifa zilizomo kwenye data inayohusishwa na mawasiliano maalum yaliyotolewa kwa njia ya mfumo wa kompyuta; au (b) kukusanya au kurekodi data kwa kompyuta kwa njia ya kiufundi.

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents