Na.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 64 mtoa huduma anaisambaza au kuhifadhi; (b) hatafuta maelezo au mazingira yanayoonyesha shughuli zinazofanywa kinyume na sheria. (2) Waziri anaweza kuweka masharti yanayohusu utaratibu wa watoa huduma kwa ajili ya(a) kutoa taarifa kwa mamlaka husika ya umma kuhusiana na shughuli zilizo kinyume na sheria zilizofanywa au taarifa inayotolewa na watumiaji wa huduma zao; na (b) kuzipatia mamlaka husika, kwa kuomba, taarifa zitakazowezesha kuwatambua watumia huduma. (3) Mtoa huduma hatawajibika kwa uwekaji wazi wa data iliyotolewa kihalali kwa mtu wa tatu baada ya kuthibitisha kwamba: (a) mtu huyo wa tatu alitenda hivyo pasipo mtoa huduma ya mtandao kufahamu; au (b) mtoa huduma alitekeleza wajibu unaostahili na alitumia ujuzi ili kuzuia uwekwaji wazi wa data hizo. (4) Endapo mtoa huduma atakuwa na uelewa juu ya taarifa au kitendo cha kihalifu kwenye mfumo wa kompyuta ambao upo chini ya udhibiti wake, atatakiwa(a) kuondoa taarifa kwenye mfumo wa kompyuta uliyo chini ya udhibiti wa mtoa huduma; (b) kusimamisha au kusitisha huduma inayohusu taarifa au kitendo hicho; (c) kutaarifu mamlaka husika juu ya kitendo au taarifa hiyo, maelezo husika na utambuzi wa mhusika anayepewa huduma. Mtoa huduma 40.-(1) Mtoa huduma ya uwezo wa kuingia kwenye ya kuingia kwenye mfumo mfumo hatawajibika kwa kurusha au kuendesha mfumo wa kompyuta kwa ajili ya mtu wa tatu katika njia ya mawasiliano yakielektroniki ambayo yeye ni mtoa huduma tu ya kuwezesha kuingia kwenye mfumo wa

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents