Na 11
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,
2022
na kwamba pamoja na hayo, mchakataji atakuwa na
wajibu wa kuhakikisha anazingatia viwango vya usalama
sawa na vinavyoelekezwa na Sheria hii.
(5) Mkusanyaji atakuwa na wajibu wa kuitaarifu
Tume, haraka iwezekanavyo, kuhusu uvunjifu wa usalama
unaoathiri taarifa binafsi zinazochakatwa kwa niaba ya
mkusanyaji.
Uhifadhi na
utoaji wa taarifa
binafsi
28.-(1) Endapo mkusanyaji atatumia taarifa binafsi
kwa madhumuni maalum kama ilivyoainishwa katika
kifungu cha 25, atatakiwa kuhifadhi taarifa hizo kwa
kipindi kilichoainishwa katika sheria zilizopo au kwa
kipindi ambacho kitaainishwa katika kanuni ili
kuhakikisha kuwa mhusika wa taarifa anapata fursa ya
kuzipata taarifa hizo pale atakapozihitaji.
(2) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (1), Waziri
anaweza, kwa kanuni, kuanisha taratibu za uhifadhi na
uteketezaji wa taarifa binafsi alizonazo mkusanyaji kwa
kuzingatia madhumuni ya uhifadhi.
Usahihishaji wa
taarifa binafsi
29.-(1) Endapo katika nyaraka au jalada ambalo
upatikanaji wake umeruhusiwa chini ya Sheria hii kuna
taarifa binafsi ambazo mhusika wa taarifa hizo anadai
kuwa(a) hazijakamilika, sio sahihi au zinapotosha; au
(b) haziendani na dhumuni la uhifadhi wa taarifa
husika,
mkusanyaji, kwa kuzingatia utaratibu utakaoainishwa
katika kanuni, na baada ya kupokea maombi ya mhusika
wa taarifa na kujiridhisha nayo, anaweza kurekebisha
taarifa hizo.
(2) Mkusanyaji, wakati wa kufanya marekebisho
kwenye taarifa binafsi chini ya kifungu hiki, atahakikisha
kuwa hafuti kumbukumbu ya maandishi ya nyaraka kama
ilivyokuwa kabla ya marekebisho.
(3) Endapo mkusanyaji hataridhika na sababu za
maombi chini ya kifungu kidogo cha (1), anaweza kukataa
kufanya marekebisho yoyote kwenye taarifa binafsi na
kumtaarifu mwombaji sababu za kukataa maombi.
16
Select target paragraph3
Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents