Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 na kwamba pamoja na hayo, mchakataji atakuwa na wajibu wa kuhakikisha anazingatia viwango vya usalama sawa na vinavyoelekezwa na Sheria hii. (5) Mkusanyaji atakuwa na wajibu wa kuitaarifu Tume, haraka iwezekanavyo, kuhusu uvunjifu wa usalama unaoathiri taarifa binafsi zinazochakatwa kwa niaba ya mkusanyaji. Uhifadhi na utoaji wa taarifa binafsi 28.-(1) Endapo mkusanyaji atatumia taarifa binafsi kwa madhumuni maalum kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 25, atatakiwa kuhifadhi taarifa hizo kwa kipindi kilichoainishwa katika sheria zilizopo au kwa kipindi ambacho kitaainishwa katika kanuni ili kuhakikisha kuwa mhusika wa taarifa anapata fursa ya kuzipata taarifa hizo pale atakapozihitaji. (2) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (1), Waziri anaweza, kwa kanuni, kuanisha taratibu za uhifadhi na uteketezaji wa taarifa binafsi alizonazo mkusanyaji kwa kuzingatia madhumuni ya uhifadhi. Usahihishaji wa taarifa binafsi 29.-(1) Endapo katika nyaraka au jalada ambalo upatikanaji wake umeruhusiwa chini ya Sheria hii kuna taarifa binafsi ambazo mhusika wa taarifa hizo anadai kuwa(a) hazijakamilika, sio sahihi au zinapotosha; au (b) haziendani na dhumuni la uhifadhi wa taarifa husika, mkusanyaji, kwa kuzingatia utaratibu utakaoainishwa katika kanuni, na baada ya kupokea maombi ya mhusika wa taarifa na kujiridhisha nayo, anaweza kurekebisha taarifa hizo. (2) Mkusanyaji, wakati wa kufanya marekebisho kwenye taarifa binafsi chini ya kifungu hiki, atahakikisha kuwa hafuti kumbukumbu ya maandishi ya nyaraka kama ilivyokuwa kabla ya marekebisho. (3) Endapo mkusanyaji hataridhika na sababu za maombi chini ya kifungu kidogo cha (1), anaweza kukataa kufanya marekebisho yoyote kwenye taarifa binafsi na kumtaarifu mwombaji sababu za kukataa maombi. 16

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents