Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 uchunguzi ya Sheria hii, Tume, katika namna itakayoainishwa katika kanuni, inapaswa kumpa notisi ya uchunguzi mkusanyaji au mchakataji anayehusika na malalamiko na nia ya kufanya uchunguzi katika suala hilo. Usiri wa uchunguzi 41.-(1) Uchunguzi wa malalamiko chini ya Sheria hii utafanyika kwa siri. (2) Mkurugenzi Mkuu au mtu yeyote anayefanya kazi kwa niaba yake ya kupokea taarifa binafsi zinazohusu uchunguzi wowote chini ya Sheria hii au sheria nyingine yoyote, atapaswa kukidhi matakwa yoyote ya kiusalama kwa kuchukua kiapo cha usiri kinachopaswa kuchukuliwa na watu ambao wanatekeleza majukumu kama hayo. Mamlaka ya Tume wakati wa uchunguzi 42.-(1) Wakati wa kuchunguza malalamiko, Tume itakuwa na mamlaka ya(a) kuita na kumtaka mtu kuhudhuria mbele ya Tume; (b) kupokea na kukubali ushahidi na taarifa nyingine, kwa kiapo au kwa hati ya kiapo au vinginevyo; (c) kuingia katika jengo lolote linalomilikiwa na mkusanyaji au mchakataji yeyote kwa ajili ya kujiridhisha endapo jengo hilo linakidhi mahitaji ya usalama; (d) kumhoji mtu yeyote au kuondoka na kifaa chochote chenye taarifa binafsi katika jengo lolote alimoingia kwa mujibu wa aya (c); na (e) kuchunguza au kupata nakala za, au dondoo kutoka kwenye vitabu, nyaraka au kumbukumbu nyingine zilizopatikana katika jengo alimoingia kwa mujibu wa aya (c) zenye suala lolote linalohusika na uchunguzi. (2) Wakati wa uchunguzi wa malalamiko chini ya kifungu hiki, mlalamikaji na mkusanyaji au mchakataji anayelalamikiwa anaweza kupewa nafasi ya kufanya mawasilisho kwa Tume. 24

اختر الفقرة المستهدفة3

الاتصال بفقرة
Connect to an entity
Disable highlights
أضف إلى جدول المحتويات