Na 11
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,
2022
(3) Bila kujali sheria nyingine yoyote, Tume
inaweza kuchunguza taarifa binafsi iliyorekodiwa katika
namna yoyote inayohifadhiwa na mkusanyaji au
mchakataji, na katika kufanya hivyo, Tume haitazuiliwa
kupata taarifa yoyote.
(4) Nyaraka au andiko lolote litakalotolewa chini
ya kifungu hiki na mkusanyaji au mchakataji au mtu
mwingine yeyote, litarejeshwa na Tume ndani ya siku
kumi za kazi baada ya maombi kuwasilishwa kwa Tume
na mkusanyaji au mchakataji au mtu huyo, lakini hakuna
chochote katika kifungu kidogo hiki kitakachoizuia Tume
kuhitaji nyaraka au andiko hilo kuwasilishwa tena kwa
mujibu wa kifungu hiki.
Kuizuia Tume
Kutumia
msaada wa mtu
au mamlaka
nyingine
43. Mtu ambaye, kuhusiana na utekelezaji wa
mamlaka iliyotolewa chini ya Sheria hii(a) ataizuia au kuikwamisha Tume katika
utekelezaji wa mamlaka yake;
(b) atashindwa kutoa msaada au taarifa
zilizoombwa na Tume;
(c) atakataa kuiruhusu Tume, inapotekeleza
majukumu yake, kuingia katika majengo yoyote
au kuondoka na nyaraka au kifaa chochote
chenye taarifa binafsi; au
(d) ataipa Tume taarifa yoyote ambayo ni ya uongo
au ya kupotosha,
anatenda kosa na endapo atatiwa hatiani atawajibika kulipa
faini isiyopungua shilingi laki moja na isiyozidi shilingi
milioni tano au kifungo kisichozidi miaka miwili au vyote
kwa pamoja.
44.-(1) Kwa madhumuni ya kukusanya taarifa au kwa
uchunguzi wowote chini ya Sheria hii, Tume inaweza
kushirikiana au kumtumia mtu au mamlaka nyingine
yoyote kama itakavyoona inafaa kwa ajili ya kuisaidia
Tume katika utekelezaji wa majukumu yake.
(2) Mtu au mamlaka nyingine itakayoshirikishwa
au kutumiwa na Tume kwa mujibu wa kifungu kidogo cha
(1), itakuwa na mamlaka sawa na mamlaka iliyo nayo
Tume katika kutekeleza mamlaka ya uchunguzi kwa
mujibu wa Sheria hii.
25
اختر الفقرة المستهدفة3
الاتصال بفقرة
Connect to an entity
Disable highlights
أضف إلى جدول المحتويات