Na 11
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,
2022
Notisi ya
utekelezaji
45.-(1) Pale ambapo Tume imeridhika kuwa mtu
ameshindwa kuzingatia kifungu chochote cha Sheria hii,
Tume inaweza kutoa notisi ya utekelezaji kwa mtu huyo
ikimtaka kuchukua hatua za kurekebisha mapungufu ndani
ya kipindi kitakachoainishwa katika notisi.
(2) Notisi ya utekelezaji itakayotolewa chini ya
kifungu kidogo cha (1)(a) itaainisha kifungu cha Sheria hii ambacho
kimekiukwa;
(b) itaainisha hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili
kukabiliana au kuondoa tatizo husika;
(c) itabainisha kipindi ambacho hatua husika
zitapaswa kutekelezwa ambacho hakitapungua
siku ishirini na moja; na
(d) itaeleza haki ya kukata rufaa.
Notisi ya
adhabu
46.-(1) Pale ambapo Tume itajiridhisha kuwa mtu
ameshindwa au anashindwa kuzingatia notisi ya
utekelezaji iliyotolewa chini ya kifungu cha 45, Tume
inaweza kutoa notisi ya adhabu inayomtaka mtu kulipa
kwa Tume faini ya kiasi kitakachoainishwa kwenye notisi.
(2) Katika kuamua iwapo inaweza kutoa notisi ya
adhabu kwa mtu na kuamua kiasi cha adhabu, Tume
itapaswa, kadiri itakavyoona muhimu, kuzingatia(a) aina na uzito wa ukiukwaji, na muda ambao
ukiukwaji huo umekuwa ukiendelea;
(b) endapo ukiukwaji umefanywa kwa nia ovu au
uzembe;
(c) hatua yoyote iliyochukuliwa na mkusanyaji au
mchakataji
ili
kupunguza
madhara
waliyoyapata wahusika wa taarifa zikiwemo
hatua za kiufundi na za kiutawala;
(d) ukiukwaji aliowahi kufanya mkusanyaji au
mchakataji awali;
(e) kiwango cha ushirikiano alichoonesha kwa
Tume kwa lengo la kurekebisha ukiukwaji na
kupunguza athari hasi za ukiukwaji zinazoweza
kujitokeza;
(f) aina ya taarifa binafsi zilizoathiriwa na
ukiukwaji;
26
اختر الفقرة المستهدفة3
الاتصال بفقرة
Connect to an entity
Disable highlights
أضف إلى جدول المحتويات