47 No.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 (2) Mtu ambaye(a) anawasilisha, anafichua au anasambaza data kompyuta, programu ya kompyuta, ishara ya kuingilia au anaagiza mtu ambaye hajaidhinishwa; (b) kwa makusudi na kinyume cha sheria anapokea data kompyuta ambayo haijaidhinishwa, ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni mbili au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria au yoyote iliyokubwa, au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja. (3) Mtu ambaye kwa makusudi na isivyo halali ataharibu au atabadili data yoyote ya kompyuta, iwapo data hiyo inatakiwa kutunzwa kisheria au ni ushahidi kwenye shauri lolote chini ya Sheria hii kwa(a) kuharibu au kubadilisha data, programu au aina nyingne yoyote ya taarifa iliyoko ndani au nje ya mfumo wa kompyuta; (b) anawasha, anaingiza au anapakua programu ambayo imetengenezwa kwa lengo la kuharibu, au kubadilisha data, programu au aina nyingine yoyote ya taarifa iliyoko ndani au nje ya mfumo wa kompyuta; au (c) anatengeneza, anabadilisha au anaharibu namba ya siri, namba binafsi ya utambulisho au namna inayotumika kuingika kwenye mfumo wa kompyuta, atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni ishirini au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au yoyote iliyokubwa, au

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents