Na 11
Katazo la
uchakataji wa
taarifa binafsi
nyeti
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,
2022
30.-(1) Mtu hatachakata taarifa binafsi nyeti bila
ridhaa ya maandishi ya mhusika wa taarifa.
(2) Ridhaa chini ya kifungu kidogo cha (1)
inaweza kuondolewa na mhusika wa taarifa wakati
wowote na bila maelezo au gharama yoyote.
(3) Waziri, kupitia kanuni, anaweza kuamua
mazingira ambayo katazo la uchakataji wa taarifa binafsi
lililoelezwa chini ya kifungu hiki halitaweza kuondelewa
hata kwa ridhaa ya mhusika wa taarifa.
(4) Endapo mhusika wa taarifa ambaye ridhaa
yake inaombwa kwa madhumuni ya Sheria hii ni mtoto,
mtu asiyekuwa na akili timamu au mtu mwingine yeyote
asiye na uwezo wa kutoa ridhaa, ridhaa ya mtu huyo
itapatikana kutoka kwa mzazi, mlezi, mrithi, wakili wake
au mtu mwingine yeyote anayetambulika kisheria kwa
niaba yake anayepaswa kutoa ridhaa.
(5) Kifungu kidogo cha (1) hakitatumika iwapo(a) uchakataji ni muhimu kwa uzingatiaji wa sheria
nyingine;
(b) uchakataji ni muhimu kulinda maslahi muhimu
ya mhusika wa taarifa au ya mtu mwingine,
iwapo mhusika wa taarifa hawezi kutoa ridhaa
yake au hajawakilishwa na mwakilishi wake
kisheria;
(c) uchakataji ni muhimu kwa ajili ya kufungua,
uendeshaji au utetezi wa madai ya kisheria;
(d) uchakataji unahusiana na taarifa binafsi
zilizowekwa wazi kwa umma na mhusika wa
taarifa;
(e) uchakataji ni muhimu kwa madhumuni ya tafiti
ya kisayansi na Tume, kwa miongozo maalum,
imeainisha mazingira ambayo uchakataji huo
unaweza kufanyika; au
(f) uchakataji ni muhimu kwa madhumuni ya
kitabibu kwa maslahi ya mhusika wa taarifa, na
taarifa binafsi nyeti zinazohusika, zinachakatwa
chini ya usimamizi wa mtaalamu wa afya kwa
mujibu wa sheria inayosimamia huduma hizo.
SEHEMU YA TANO
17
Select target paragraph3
Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents