Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 USAFIRISHAJI WA TAARIFA BINAFSI NJE YA NCHI Kusafirisha taarifa binafsi kwenda nchi yenye ulinzi wa kutosha wa taarifa binafsi 31.-(1) Tume inaweza, kwa kuzingatia masharti ya Sheria hii, kuzuia usafirishaji wa taarifa binafsi kwenda nje ya nchi. (2) Taarifa binafsi itasafirishwa kwenda nchi yenye mfumo wa kisheria unaotoa ulinzi wa kutosha wa taarifa binafsi pale ambapo(a) mpokeaji atabainisha kuwa taarifa binafsi ni muhimu kwa utekelezaji wa jukumu lenye maslahi ya umma au kwa mujibu wa shughuli halali za mkusanyaji wa taarifa binafsi; au (b) mpokeaji atabainisha umuhimu wa kusafirisha taarifa na hakuna sababu ya kudhani kwamba maslahi halali ya mhusika wa taarifa yanaweza kuathiriwa na usafirishaji au uchakataji katika nchi inayopokea. (3) Mkusanyaji atapaswa, bila kujali kifungu kidogo cha (2), kufanya tathmini ya awali ya umuhimu wa usafirishaji wa taarifa binafsi. (4) Mpokeaji atahakikisha kuwa umuhimu wa usafirishaji wa taarifa binafsi unaweza kuthibitishwa baadaye. (5) Mkusanyaji atahakikisha kwamba mpokeaji anachakata taarifa binafsi kwa madhumuni ambayo yalipelekea kusafirishwa kwa taarifa husika pekee. Kusafirisha kwenda nchi isiyo na ulinzi wa kutosha wa taarifa binafsi 32.-(1) Taarifa binafsi zitasafirishwa kwenda nchi nyingine tofauti na zile zilizotajwa katika kifungu cha 31, ikiwa ulinzi wa kutosha umehakikishwa katika nchi ya mpokeaji na taarifa inasafirishwa kwa dhumuni la kuruhusu uchakataji ulioruhusiwa kufanyika na mkusanyaji. (2) Utoshelevu wa kiwango cha ulinzi unaotolewa na nchi nyingine utatathminiwa kwa kuzingatia(a) mazingira yote yanayozunguka usafirishaji wa taarifa binafsi husika; (b) aina ya taarifa binafsi; (c) madhumuni na muda wa uchakataji unaopendekezwa; 18

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents