65 No.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 kompyuta au kuendesha vifaa kupitia mfumo wa kompyuta ulio chini ya mamlaka yake kwa masharti kwamba mtoa huduma(a) haanzishi urushaji mawasiliano; (b) hachagui mpokeaji wa mawasiliano; au (c) hachagui au habadilishi data iliyoko kwenye mawasiliano. (2) Mawasiliano na utoaji wa uwezo wa kuingia kwenye mfumo wa kompyuta yaliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha ( 1) utajumuisha, utunzaji wa taarifa iliyosambazwa kwa madhumuni ya kuendeleza mawasiliano kwenye mfumo wa kompyuta kwa njia inayojiendesha yenyewe kwa kupitia mtu kati na kwa muda kwa kuzingatia kwamba mawasiliano yanafanyika kwa(a) madhumuni ya kuendesha na kusambaza taarifa katika mfumo wa kompyuta; (b) namna ambayo kwa kawaida haiwezi kupatikana isipokuwa tu kwa mpokeaji mlengwa;na (c) muda ambao sio mrefu sana zaidi ya muda unaofaa kuwasilisha ujumbe husika kwa mlengwa. Mtunza Data 41-(1) Mtunza data hatawajibika na taarifa zilizohifadhiwa kwa maombi ya mtumiaji wa huduma hiyo, kwa masharti kwamba(a) anaondoa au kusitisha mara moja upatikanaji wa taarifa baada ya kupokea amri kutoka taasisi yenye mamlaka au mahakama ya kuondoa taarifa zilizo kinyume cha sheria; au (b) baada ya kufahamu kuwa taarifa iliyohifadhiwa iko kinyume cha sheria ataitaarifu mara moja taasisi husika. (2 ) Kifungu kidogo cha ( 1) hakitatumika pale

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents