Na.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 66 ambapo mpokeaji anafanya hivyo chini ya mamlaka ya mtoa huduma. Mhifadhi data kwa muda mfupi 42. Mtoa huduma ya kuhifadhi data hatawajibika kwa ajili ya utunzaji wa taarifa ikiwa(a) habadilishi taarifa; (b) anatekeleza masharti ya utoaji wa uwezo wa kuingia kwenye mfumo; (c) anazingatia kanuni zinazohusu na uboreshaji wa taarifa; (d) haiingiliani na matumizi halali ya teknolojia inayotambulika na wengi na inayotumika sokoni kupata data kwa ajili ya matumizi ya taarifa hiyo; na (e) anachukua hatua za haraka kuondoa au kusitisha matumizi ya au kufikiwa kwa taarifa ambayo imetunzwa baada ya kupokea taarifa kamili kwamba taarifa iliyo kwenye chanzo cha mawasiliano imeondolewa kutoka kwenye mtandao, au ufikiwaji wake umesitishwa au matumizi yake yamesitishwa, au kwamba mahakama au mamlaka husika imeamuru itolewe au isitishwe. Mtoa huduma ya kuunganisha tovuti 43. Mtoa huduma ya kuunganisha tovuti hatawajibika kwa taarifa aliyounganisha iwapo(a) haraka iwezekanavyo anaondoa au anasitisha matumizi ya taarifa baada ya kupokea amri kutoka kwa mamlaka husika ya kuondoa kiunganishi hicho; na

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents